Thursday 10 September 2015

MIKUMI HIFADHI MASHUHURI NCHINI TANZANIA



  Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
   Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
-Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.
-Wanyama wengine wengi hukimbilia katika eneo la miombo nyakati za mvua ambako unaweza kuwaona katika safu za milima. Hapo makundi makubwa ya nyati katika ukanda wa miombo wanaweza kuonekana.
-Kwa upande wa ndege, wakati wa mvua huongezeka na kufikia zaidi ya aina 300. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, nyakati hizi kunakuwepo na makundi ya ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia ambayo, huungana na makundi ya ndege wakazi  kama vile chole.
-Makundi makubwa ya viboko, pundamilia na nyumbu huonekana katika eneo hili

No comments: