Friday 18 April 2014

KIVUTIO CHA UTALII NDANI YA CHUO KIKUU CHA SOKOINE


     Vivutio vya utalii ni  sehemu au kitu chochote kinacho mvutia mtalii  kutembelea na kuona  kitu au sehemu hiyo. Kivutio hicho chaweza kuwa wanyama, makumbusho ya kale au tamaduni za jamii fulani.
      Kutokana na maana hiyo basi nimeona  leo tena kubaki pale pale mji kasoro bahari (Morogoro) ndani ya Chuo kikuu cha Sokoine katika kampusi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu, na kuangaza katika moja ya kivutio  ambacho chawezekana hakitambuliki na wengi  na hicho si kingine ni “ South  African graveyard”.


 
  South African graveyard haya ni makaburi ya watu Africa ya kusini walioishi Tanzania, mjini Morogoro wakati wa kugombania uhuru wa  nchi yao chini ya kiongozi wao Solomon Mahlangu ,lakini vilevile  ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Afrika ya kusini.

  
  Lakini katika dhana ya Utalii makaburi hayo ni moja ya kivutio cha kihostoria ambacho kikihifadhiwa na kutangazwa kama moja ya vivutio vya utalii vilivyopo Morogoro, kwa kiasi kikubwa  kinaweza kuchangia pato la mji huo na pia  kukifanya Chuo Kikuu cha Sokoine  kujulikana











 




 Hivyo basi ni Jukumu la utawala wa chuo hicho ikishirikiana na serikali ya wanafunzi (SUASO) pamoja na wanafunzi wa shahadaya utalii waliopo chuoni hapo ili  kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa kivutio hicho kinatunza ili kiweze kutumika kama kivutio cha Utalii.









No comments: