Sunday, 9 August 2015

Historia na uzuri wa Kisiwa cha Mafia


 
Mafia ni funguvisiwa cha Kitanzania pamoja na jina la kisiwa kikubwa ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki 130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni 16 km.
Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 20 km na upana wa 8km; eneo lake ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa kikuu.
Wilaya
Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni.
Tarafa za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo:

Uchumi

   Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na nazi, chokaa na samaki. Kuna utalii inayosifiwa sana lakini idadi ya wageni ni kidogo. Hasa Waitalia wanapenda kutembelea Mafia kwa sababu ya jina la kisiwa. Mafia imemaanisha shirika la jinai la kuhofiwa lenye historia ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
Historia
    Kihistoria Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani.Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka Sultani ya Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. 1915 Waingereza Baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika sio tena Zanzibar waliteka kisiwa wakishambulia manowari ya Kijerumani mdomoni wa mto Rufiji kutoka Mafia.

No comments: