Hifadhi ya Katavi
ni moja ya hifadhi za taifa ambayo iko juu ya uwanda mpana wa mafuriko
magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Rukwa. Ina ukubwa wa eneo la kilometa za
mraba 4471
Madhari katika hifadhi
·
Maeneo ya majimaji yenye majani
·
Mimea jamii ya mitende na
·
Mto Katuma
Hifadhi hii inasifika kwa:
Idadi kubwa ya mamba na viboko.Pia
wanyama kama simba na chui hawana shida ya mawindo kwani katika himaya yao kuna
makundi ya swala, nyamela topi wa miguu mieupe, pundamilia na nyati.
Kuna ainazipatazo 400 za ndege
waliozagaa katika miti ya acacia, kingo za mto, mabwawa na makundi kadhaa ya mwari yanayoambaa ziwani. Nikawaida kuyaona makundi makubwa ya tembo yalkila
majani katika mabwawa huku miili yao ikiwa imefunikwa na maji na magugu
Namna ya kufikaa katika hifadhi
- Inafikika kwa ndege kutoka miji ya Dar es salaam na Arusha
- Kwa gari kutoka mji wa Mbeya au kupitia mji wa Kigoma
No comments:
Post a Comment