Maeneo yanayozunguka Ziwa Natron
yana baadhi ya mazingira ya kushangaza zaidi barani Afrika. Mazingira hayo ni
pamaoja na mchanganyiko wa maeneo mpana ya wazi na tambarare, miinuko, Mlima mkubwa
wa volkano pamoja na ziwa lenyewe lenye asili ya madini soda yenye rangi
mbalimbali, ni dhahiri kwamba eneo hili ni la kuvutia na kupendeza.
Umuhimu wa ziwa hili katika ukanda wa Afrika Mashariki unatokana na
ukweli kwamba ndio sehemu pekee katika ukanda huu ambapo panatoa fursa ya
ndege aina ya flamingo kuzaliana kwa wingi.