Monday, 19 October 2015

ZIWA NATRON LINA MAENEO YA KUSHANGAZA BARANI AFRIKA



Maeneo yanayozunguka Ziwa Natron yana baadhi ya mazingira ya kushangaza zaidi barani Afrika. Mazingira hayo ni pamaoja na mchanganyiko wa maeneo mpana ya wazi na tambarare, miinuko, Mlima mkubwa wa volkano pamoja na ziwa lenyewe lenye asili ya madini soda yenye rangi mbalimbali, ni dhahiri kwamba eneo hili ni la kuvutia na kupendeza.
Umuhimu wa ziwa hili katika ukanda wa Afrika Mashariki unatokana na ukweli kwamba ndio sehemu pekee katika ukanda huu ambapo panatoa fursa ya ndege aina ya flamingo kuzaliana kwa wingi.


No comments: