Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ni maarufu duniani
kutokana na mandhari nzuri ya Mlima Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu kuliko
yote Afrika na inapatikana katika nchi ya Tanzania . Hifadhi hii ina ukubwa wa
kilometa za mraba 755 na iko umbali wa kilometa 45 kutoka Moshi mjini.Kilele
cha Kibo chenye urefu wa mita 5895 (futi
19340) ndio kivutio kikubwa kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi kutokana na
kufunikwa na theluji. Safari ya kupanda mlima huu humpitisha mpandaji katika
kanda za hali ya hewa tofauti kuanzia ile ya nchi za tropiti hadi arktiki.
Mlima huu ni moja kati ya milima ambayo kilele chake
hufikiwa kwa urahisi na hivyo kuwa kivutio kikubwa kwa wapanda milima kutoka
kila pande za dunia.
Zaidi ya watalii 20,000 hupanda mlima huu kila mwaka
wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na Watanzania. Mpandaji wa mlima huu
huhitaji angalau siku tano, siku tatu kupanda na siku mbili kuteremka.
Kuna njia sita ya kupanda mlima Kilimanjaro hadi
kileleni.
- Njia iliyo rahisi na maarufu zaidi ni ile ya
kuanzia lango la Marangu, ambako ndiyo makao makuu ya hifadhi.
Wanyama kadhaa hupatikana katika msitu unaozunguka
Mlima Kilimanjaro wakiwemo mbega, nyani, nyati, chui, tembo, swala na ndege.
.
Wakati mzuri wa
kutembelea hifadhi
Kuanzia mwezi Desemba hadi februari, na pia mwezi
Julai na Septemba (ingawa wakati huu ni baridi zaidi)