Thursday, 18 June 2015

Hifadhi ya Arusha

   ADVERTISE WITH US: +2250653683428
          Email: teresiamsanga@yahoo.com




  Hifadhi ya Arusha inapatikana katika mji wa Arusha nchini Tanzania. Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 552, iko umbali wa kilometa 32 kutoka katika mji wa kitalii wa Arusha.
Maeneo makubwa na muhimu ya hifadhi
  • Bonde la Ngurdoto
  • Maziwa ya Momela
  • Mlima Meru wenye urefu wa meta 4566 (futi 14990) hali inayofanya hifadhi kuwa na mazingira ya baridi. 
  • Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama jamii ya tumbili wajulikanao kama mbega weusi na weupe. Wanyama wengine wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi hii ni pamoja na twiga, pundamilia, nyati na digidigi. Aidha unaweza kuwaona chui wakibarizi katika vivuli vya matawi ya miti inayokingwa na maanguko ya maji huku makundi kadhaa ya batamaji yakitafuta wadudu katika maziwa ya Momela.
Zaidi ya aina 400 za ndege wamethibitika kupatikana ndani ya hifadhi hii.
Mambo yanayoweza kufanyika ndani ya hifadhi hii
Safari za miguu na kupanda mlima Meru ni moja ya burudani muhimu katika hifadhi hii, na mpandaji anahitaji siku 3-4 za kupanda mlima.
Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ni kati ya mwezi Juni na Februari ingawa mvua inaweza kunyesha mwezi novemba

Bonde la Ngurutodo


No comments: