Thursday 10 April 2014

" ZITUMIKE NJIA MBADALA KUKOMESHA UJANGILI"

Meno ya ndovu yakiteketezwa
   Kamati Tendaji Umoja wa Wabunge  wa Uhifadhi na matumizi Endelevu ya wanyamapori,imebaini Tanzania inapaswa kutumia njia tatu mbadala zitakazodhibiti ujangili.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo Riziki Lulinda,maazimio hayo yametokana na kikao  cha kamati hiyo kilichoketi Mjini Dodoma kuchambua sheria ya Uhifadhi Wanyamapori ya mwaka 2009.
  Alisema wamebani upungufu karika sera ya uhifadhi wa wanyamapori kwamba serikali  imeshindwa kuonyesha  namna itakavyoshirikiana na wananchi wanaoishi katika   maeneo yenye  hifadhi na yanayozunguka mapori ya Akiba  katika majukumu ya uhifadhi. Alisema wananchi hawajapewa elimu sahihi  inayoonesha umuhimu wa wanyamapori kwa uchumi wao na Taifa na sera imeshindwa kuonyesha mbinu na mikakati au mipango ya kuondoa au kupunguza ugomvi kati ya wafugaji , wakulima na hifadhi za Taifa.
   Alisema Taifa linapaswa kudhibiti masoko yanayotumika kwa biashara haramu ya nyara za Taifa na kudhibiti uwindaji haramu katika hifadhi. 
“Katika uchambuzi wa tatizo la msingi  la ujangili hapa nchini kamati imebaini kuwa ujangili ni sawa na mchezo wa paka na panya “, alisema  Lulinda.Alisema kufikia mkakati  wa kukabiliana  na tatizo la ujangili nchini kamati  ilibaini  kuwa kama Taifa tunaitaji kuainisha  maeneo tunayowaza kuwaona au kuwapata majangili na ili kufanikisha hilo tunahitaji wataalamu  wa uchunguzi.
 
 “Iwapo ili litafanyika  wananchi watashiriki kuonyesha  maeneo wanayojificha majangili na hii ni kwasababu majangili huhitaji msaada wa wananchi kupata  silaha, chakula , maji na zana nyingine za kufanikisha ujangili” Aisema Riziki. 

No comments: