Mafia ni funguvisiwa cha Kitanzania pamoja na
jina la kisiwa kikubwa ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya
Mashariki
130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake
na bara ni 16 km.
Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 20 km na upana wa 8km; eneo lake
ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana
na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa
kikuu.
Wilaya
Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkuu na makao makuu ya wilaya
ni Kilindoni.
Tarafa
za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo:
Uchumi
Wakazi
walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja
na nazi, chokaa na samaki. Kuna utalii inayosifiwa sana lakini idadi ya wageni
ni kidogo. Hasa Waitalia wanapenda kutembelea Mafia kwa sababu ya jina la
kisiwa. Mafia imemaanisha shirika la jinai la kuhofiwa lenye historia ndefu
katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
Historia
Kihistoria
Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji
ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani.Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia
kutoka Sultani ya Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. 1915 Waingereza Baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika sio tena Zanzibar waliteka kisiwa
wakishambulia manowari ya Kijerumani mdomoni wa mto Rufiji kutoka Mafia.