Friday, 18 April 2014

KIVUTIO CHA UTALII NDANI YA CHUO KIKUU CHA SOKOINE


     Vivutio vya utalii ni  sehemu au kitu chochote kinacho mvutia mtalii  kutembelea na kuona  kitu au sehemu hiyo. Kivutio hicho chaweza kuwa wanyama, makumbusho ya kale au tamaduni za jamii fulani.
      Kutokana na maana hiyo basi nimeona  leo tena kubaki pale pale mji kasoro bahari (Morogoro) ndani ya Chuo kikuu cha Sokoine katika kampusi ya Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu, na kuangaza katika moja ya kivutio  ambacho chawezekana hakitambuliki na wengi  na hicho si kingine ni “ South  African graveyard”.


 
  South African graveyard haya ni makaburi ya watu Africa ya kusini walioishi Tanzania, mjini Morogoro wakati wa kugombania uhuru wa  nchi yao chini ya kiongozi wao Solomon Mahlangu ,lakini vilevile  ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Afrika ya kusini.

  
  Lakini katika dhana ya Utalii makaburi hayo ni moja ya kivutio cha kihostoria ambacho kikihifadhiwa na kutangazwa kama moja ya vivutio vya utalii vilivyopo Morogoro, kwa kiasi kikubwa  kinaweza kuchangia pato la mji huo na pia  kukifanya Chuo Kikuu cha Sokoine  kujulikana











 




 Hivyo basi ni Jukumu la utawala wa chuo hicho ikishirikiana na serikali ya wanafunzi (SUASO) pamoja na wanafunzi wa shahadaya utalii waliopo chuoni hapo ili  kutafuta njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa kivutio hicho kinatunza ili kiweze kutumika kama kivutio cha Utalii.









Monday, 14 April 2014

MCHANGO WA WANAFUNZI WA SHAHADA YA UTALII 2011-2013 (SUA) KATIKA KUKUZA UTALII WA NDANI.


        Leo kwenye makala yetu tunaangaza katika Utalii wa ndani. Jicho letu limeelekea mji kasoro bahari((Morogoro) katika Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine
Sokoine University of Agriculture 





 
 Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine ni chuo kinacho toa shahada za kilimo na nyinginezo lakini takribani miaka mitatu iliyo pita chuo hiki kilianzisha Shahada  ya Utalii.Ni kvipi basi shahada hii imesaidia kukuza utalii wa ndani?
     Wanafunzi wanaochukua Shahada ya Utalii wameonekana kuwa na muamko mkubwa wa kutembelea vivutio mbalimbali pamoja na Hifadhi za Taifa kama vile Mikumi, Kilimanjaro,Saadani, Lake Manyara na Mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro,pia  wanafunzi hao wameweza kutembelea vivutio  vingine kama vile Kaole na Ngome Kongwe huko Bagamoyo,Mapango ya Amboni pamoja na Fukwe za Ushongo zilizopo Tanga.
  Hali kadhalika wanafunzi hao hawakukosa kuwa wazalendo pia wameweza kutembelea vivutio vilivyopo katika mji wa Morogoro zikiwemo Uluguru Nature Reserve na Udzugwa Nature Reserve.Hata hivvo basi wanafunzi wachache wa mwaka wa masomo 2010-2013 waliweza kuanzisha chombo kinachoandaa trip mbalimbali kilichojulikana kama Domestic Tourism Promoters (DOTOPs).


Kilimanjaro at Uhuru peak
 Lake Manyaral













Ngorongoro conservation area
Kaole

Picha ya pamoja kaole0








0
Uluguru nature conservation














   Hivyo basi Wanafunzi wa Shahada ya Utalii wamekuwa chachu katika kukuza utalii wa ndani  kwa wakuweza kuwashawi wanafunzi wa Shahada nyingine kama vile Shahada ya Elimu na Maendeleo ya Vijiji kuwa na hari  ya kutembelea vivutio vya Utalii