Tuesday, 18 August 2015

Ziwa Eyasi ni kivutio kizuri cha Utalii nchini Tanzania


    Ziwa Eyasi ni ziwa lenye maji ya chumvi linalopatikana kati ya genge la bonde la ufa na na Milima ya Kidero. Maeneo yazungukayo ziwa Eyasi ni makazi ya kabila maarufu la Wahadzabe ambao ni moja ya makabila machae ya wawindaji yaliyobaki katika bara la Afrika. Wahadzabe wamekuwa wakiishi katika misitu ya acacia na vichaka vinavozunguka maeneo ya ziwa Eyasi kwa atakribani zaidi ya miaka 10,000 iliyopita.
Utalii unaofnyika katika eneo hili ni utalii wa kitamaduni.

Monday, 17 August 2015

Maziwe Island the best diving destination along the Eastern African Coast



   Maziwe island is a very small unvegetated island surrounded by coral reefs located about 8 kilometres south east of the town of Pangani off the northern coast of Tanzania.
       Flora and Fauna
 There is a wide diversity of marine species found in and around the island reserves. This includes over 200 species of fish, 35 genera of corals, many types of birds and a number of different sea grasses, algae and sponges. The island used to be a nesting site for endangered green sea turtles.
    Tourism activities
 Maziwe remains an ideal place for swimming, snorkeling and diving as well as research expedition, sunbathing and watching dazzling tropical fish.
The area is ideal for underwater adventures and is among the best diving destination along the Eastern African Coast with a wide variety of underwater life.

Tuesday, 11 August 2015

Mkwawa’s memorial museum building at Kalenga village - Iringa Town


Since the Germans had more sophisticated weapons that spears, bows and arrows the Hehe soldiers had, were no match for the guns the German troops had, they managed to attack the Hehe fortress at Kalenga in October 1894 and Chief Mkwawa successfully managed to escape and engaged in the German forces in guerrilla warfare for a number of years before he committed suicide. In 1898, after nine years of harassing the Germans in a series of guerrilla skirmishes, Mkwawa was cornered by the German troops, and on realizing that he was about to be arrested, he committed suicide rather than being caught red handed by the colonial German troops. As the German troops advanced, they found him dead and cut off his head which was sent to Germany, and repatriated back to the then Tanganyika territory in 1954 during British colonialism. Mkwawa’s skull now forms one of the main exhibits in the Mkwawa Memorial Museum at nearby Kalenga village.

Sunday, 9 August 2015

Historia na uzuri wa Kisiwa cha Mafia


 
Mafia ni funguvisiwa cha Kitanzania pamoja na jina la kisiwa kikubwa ndani yake inayotazama mwambao wa Afrika ya Mashariki 130 km kusini ya Daressalaam karibu na mdomo wa Mto Rufiji. Umbali wake na bara ni 16 km.
Mafia kisiwa kikuu ina urefu wa 20 km na upana wa 8km; eneo lake ni takriban 400 km². Inajulikana pia kwa jina "Chole shamba" kutokana na mji wa kale wa Chole iliyokuwepo kwenye kisiwa kidogo cha Chole mjini karibu na kisiwa kikuu.
Wilaya
Wilaya ya Mafia ni kati ya wilaya 6 za mkoa wa Pwani ikiwa na wakazi 40,801 (2002). Mji mkuu na makao makuu ya wilaya ni Kilindoni.
Tarafa za wilaya ya Mafia ni kama zifuatazo:

Uchumi

   Wakazi walio wengi ni wavuvi wanaolima pia mashamba madogo. Bidhaa za sokoni ni pamoja na nazi, chokaa na samaki. Kuna utalii inayosifiwa sana lakini idadi ya wageni ni kidogo. Hasa Waitalia wanapenda kutembelea Mafia kwa sababu ya jina la kisiwa. Mafia imemaanisha shirika la jinai la kuhofiwa lenye historia ndefu katika Italia ya kusini hadi siku ya leo.
Historia
    Kihistoria Mafia ilikuwa mahali pa miji ya kale ya utamaduni wa Waswahili kama vile miji ya Chole na Kua. Baada ya kuondoka kwa Wareno ilikuwa chini ya Sultani wa Omani.Mwaka 1892 Wajerumani walinunua Mafia kutoka Sultani ya Zanzibar ikawa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. 1915 Waingereza Baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Mafia imekuwa sehemu ya Tanganyika sio tena Zanzibar waliteka kisiwa wakishambulia manowari ya Kijerumani mdomoni wa mto Rufiji kutoka Mafia.

Monday, 3 August 2015

Sunday, 2 August 2015

Umuhimu wa Kisiwa cha Uzi kwa Serikali ya Zanzibar


  “Tourism and Leisure blog” ipo Zanzibar katika Kisiwa cha Uzi.Idadi kubwa ya wakazi wa kisiwa hiki wanategemea uvuvi kama shughuli yao ya kiuchumi.
     Lakini pia Kisiwa kidogo cha uzi kilichopo mkoa wa kusini unguja kinaweza kusaidia serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kimapato kutokana na utalii iwapo kitaendelezwa  na kutangazwa Duniani kote kutokana na kisiwa hicho kuwa na upekee wake wa kuingia na kutoka kisiwa hapo
Hivyo basi ni jukumu sasa la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari wakishirikiana na  Wizara ya Maliasili na Utalii kutafuta wawekezali ili kuweza kukifanya kisiwa hiki kuwa kivutio kikubwa cha Utalii.
 











Do you wish to visit Amboni Cave in Tanga
Contact with us: +2250653603428

Sunday, 26 July 2015

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Eden ya Afrika

    HIFADHI ya Taifa ya Serengeti inayopita katika mikoa ya Arusha,Mwanza,Mara na Shinyanga ni eneo pekee duniani lenye kundi kubwa la wanyama wanaohama katika mfumo mzima wa mlishano.
   Inasemekena neno Serengeti linatokana na neno la kimasai la sirenget lenye maana ya  uwanda mpana wa nyasi fupi,malisho mengi na maji ya kutosha pengine ndiyo maana hifadhi hiyo inapewa majina mengi kama vile bustani ya Afrika na Edeni ya Afrika kutokana na utajiri wa maliasili uliopo ndani ya hifadhi hii.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yenye ukubwa wa  kilometa za mraba 14,763 ilianzishwa mwaka 1951, ni Hifadhi ya Taifa ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226.
     Umaarufu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti  unatokana na kuwa na misururu mirefu ya nyumbu wanaohama kwa makundi  na kuvuka hata mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara nchini Kenya ambapo takwimu za TANAPA zinaonyesha kuwa kila mwaka zaidi ya nyumbu milioni moja,pundamilia 200,000, swala tomi zaidi ya 300,000 na pofu 12,000 huunga misafara ya kutafuta malisho na maji 
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti huchukuliwa kama moja ya maajabu ya dunia kutokana na tendo la uhamaji wa nyumbu kutoka kusini hadi kaskazini na kurudi, tendo ambalo linafanyika mara moja tu kwa mwaka tendo hilo linaifanya hifadhi hii kuwa Eden ya Afrika na kupendwa kutembelewa na watu wengi ulimwenguni kote. Licha ya nyumbu wanyama wengine maarufu walao nyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni chui na samba, ambapo utafiti umebaini kuwa ukubwa wa hifadhi hii umesaidia kudumisha uhai wa wanyama waliokuwa katika hatari ya kutoweka kama vile faru weusi na duma
       Watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  kutokana na makundi makubwa ya nyumbu wameifanya hifadhi hiyo kuwa maarufu Afrika mashariki na ulimwenguni kote hali iliyosababisha shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi UNESCO  kuitangaza Serengeti kuwa  eneo la urithi wa Dunia  kwa kuwa ndiyo eneo pekee ulimwenguni lililosalia kundi kubwa la wanyama wahamao.  Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ipo umbali wa kilometa 335 kutoka Arusha ikiambaa kaskazini katika mpaka na nchi ya Kenya,kwa upande wa magharibi inapakana na na ziwa Viktoria.
      Hifadhi hii inafikika kwa kukodi ndege kutokea jijini Dar es salaam,Mwanza,Kilimanjaro na Arusha pia kwa barabara kutokea Arusha,Musoma na Mwanza,wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii ili kuona uhamaji wa nyumbu ni kuanzia mwezi Desemba hadi Julai.