Tuesday, 3 November 2015

MAAJABU YA SIMBA WEUPE WA PORI LA LIPARAMBA NCHINI TANZANIA

   Katika  habari za wanyama pori inajulikana kwamba  simba weupe wanapatkana zaidi  Afrika ya kusini,Lakin pia Simba weupe wanapatikana katika nchi ya Tanzania katika pori la wanyama la Liparamba wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Pia katika pori kuna baadhi ya wanyama wanahama kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania kwa kuzingatia hifadhi hiyo iko mpakani mwa nchi hizi mbili.

MAKUMBUSHO YA TAIFA YA VIUMBE HAI YA ARUSHA


ADVERTISE WITH US CALL..0653683428

Monday, 19 October 2015

ZIWA NATRON LINA MAENEO YA KUSHANGAZA BARANI AFRIKA



Maeneo yanayozunguka Ziwa Natron yana baadhi ya mazingira ya kushangaza zaidi barani Afrika. Mazingira hayo ni pamaoja na mchanganyiko wa maeneo mpana ya wazi na tambarare, miinuko, Mlima mkubwa wa volkano pamoja na ziwa lenyewe lenye asili ya madini soda yenye rangi mbalimbali, ni dhahiri kwamba eneo hili ni la kuvutia na kupendeza.
Umuhimu wa ziwa hili katika ukanda wa Afrika Mashariki unatokana na ukweli kwamba ndio sehemu pekee katika ukanda huu ambapo panatoa fursa ya ndege aina ya flamingo kuzaliana kwa wingi.


Saturday, 12 September 2015

MOUNT RUNGWE: THE ACTIVE VOLCANIC MOUNTAIN IN MBEYA REGION



   Mount Rungwe is a potentially active volcano in the Mbeya Region of the southern highlands of Tanzania. At an altitude of 2,960 metres, it is southern Tanzania's second highest peak. Rungwe stands at the junction of the eastern and western arms of the East African Rift. It dominates the mountainous country at the north-west end of the trough that contains Lake Nyasa. The southeastern slopes of these mountains receive up to 3 metres of rainfall a year, the highest rainfall in Tanzania. The slopes are covered with a belt of tropical montane forest
  Tourism activities
Tourists uses of the Mount to trekking and photography tourism are take place

Thursday, 10 September 2015

MIKUMI HIFADHI MASHUHURI NCHINI TANZANIA



  Mikumi ni moja ya hifadhi mashuhuri na kubwa nchini Tanzania. Eneo kuu na muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko pamoja na safu za milima ambazo zinapatikanandani ya hifadhi hii. Mbuga za wazi ndizo zinazoshamiri katika uwanda wa mafuriko na kuishia katika misitu ya miombo inayofunika mabonde yaliyo chini ya hifadhi.
   Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa 3230 na ipo umbali wa kilometa 283 magharibi mwa Dar ea Salaam. Aidha hifadhi hii iko kaskazini ya mbuga ya Selouse na iko njiani unapoelekea katika hifadhi ya Udzungwa, Selouse na Ruaha kwa barabara kutoka Dar ea Salaam na Inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.
-Ndani ya hifadhi ya Mikumi kuna simba ambao huwa wanaonekana wakiwa katika himaya yao na mara nyingine wakiwa juu ya matawi ya miti ili kukwepa majimaji wakati mvua zinapototesha ardhi ambayo ina udongo wa mfinyanzi.
-Wanyama wengine wengi hukimbilia katika eneo la miombo nyakati za mvua ambako unaweza kuwaona katika safu za milima. Hapo makundi makubwa ya nyati katika ukanda wa miombo wanaweza kuonekana.
-Kwa upande wa ndege, wakati wa mvua huongezeka na kufikia zaidi ya aina 300. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, nyakati hizi kunakuwepo na makundi ya ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia ambayo, huungana na makundi ya ndege wakazi  kama vile chole.
-Makundi makubwa ya viboko, pundamilia na nyumbu huonekana katika eneo hili

Saturday, 5 September 2015

OLDONYO LENGAI MLIMA WENYE VOLKANO HAI TANZANIA



   Oldoinyo Lengai ni Mlima pekee wenye volkano hai unaopatikana Tanzania wenye urefu wa Mita 2962 kutoka usawa wa bahari. Jina hili Oldonyo Lengai lina maana ya “Mlima wa Mungu” katika lugha ya Kimasai.. Kabila la Kimasai hutumia Mlima huu kwa kufanya  matambiko wakiupa sifa za Uungu kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii yanayo wakumba kama ,njaa na magonjwa.
   Lakini pia mlima huu  hutumika kama kivutio cha Utalii, na utalii unaofanyika ni utalii wa kupanda milima. 


ADVERTISE HERE.