Vivutio vya utalii ni sehemu au kitu chochote kinacho mvutia
mtalii kutembelea na kuona kitu au sehemu hiyo. Kivutio hicho chaweza
kuwa wanyama, makumbusho ya kale au tamaduni za jamii fulani.
Kutokana na maana hiyo basi nimeona leo tena kubaki pale pale mji kasoro bahari
(Morogoro) ndani ya Chuo kikuu cha Sokoine katika kampusi ya Solomon Mahlangu
iliyopo Mazimbu, na kuangaza katika moja ya kivutio ambacho chawezekana hakitambuliki na
wengi na hicho si kingine ni “
South African graveyard”.
South African graveyard haya ni
makaburi ya watu Africa ya kusini walioishi Tanzania, mjini Morogoro wakati wa
kugombania uhuru wa nchi yao chini ya
kiongozi wao Solomon Mahlangu ,lakini vilevile
ni ishara ya mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Afrika ya kusini.
Lakini katika dhana ya Utalii makaburi hayo ni moja ya kivutio cha kihostoria ambacho kikihifadhiwa na kutangazwa kama moja ya vivutio vya utalii vilivyopo Morogoro, kwa kiasi kikubwa kinaweza kuchangia pato la mji huo na pia kukifanya Chuo Kikuu cha Sokoine kujulikana
Hivyo basi ni Jukumu la utawala wa chuo hicho
ikishirikiana na serikali ya wanafunzi (SUASO) pamoja na wanafunzi wa shahadaya
utalii waliopo chuoni hapo ili kutafuta
njia mbalimbali za kuhakikisha kuwa kivutio hicho kinatunza ili kiweze kutumika
kama kivutio cha Utalii.