Saturday, 5 April 2014

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni Mahali pekee panapohifadhi wanyamapori na binadamu

Ziwa Magadi
Ngorongoro:
Ni  eneo pekee panapohifadhi wanyamapori na binadamu, mchanga unaohama, palipogunduliwa nyayo za miguu na fuvu la binadamu wa kwanza.
Pia, kuna Ziwa Magadi ndani ya bonde refu na kubwa maarufu kwa jina la ‘Ngorongoro Crater’ lililosababishwa na milipuko ya volcano zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Mahali hapo si pengine popote, ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area Authority – NCAA) iliyoanzishwa mwaka 1959 na kukabidhiwa majukumu makuu yafuatayo:
Kuhifadhi maliasili (wanyamapori, ndege na mazingira) zilizopo, kuendeleza binadamu wenyeji (Wamaasai) na utalii katika hifadhi hiyo.

Ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,292, inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) upande wa Kaskazini Magharibi na miji ya Arusha, Moshi na Mlima Kilimanjaro upande wa Mashariki.

No comments: