Thursday 3 April 2014

MBINU MBALIMBAL ZITUMIKE KUKUZA UTALII WA NDANI.

Watalii wa ndani
Pamoja na mbinu  mbalimbali zinazotumika katika kuvitangaza vivutio na hifadhi zetu hapa nchini, utayari wa wananchi umekuwa ni mdogo katika kutembelea vivutio hivyo.Hivyo basi huu ndio muda muafaka wa wananchi na watu maarufu  kutembelea hifadhi na vivutio tulivyonavyo,i.li kukuza utalii wa ndani.
Watu maarufu kama wanasiasa, viongozi wa dini serikali wanamichezo, wasanii wa muziki na tamthilia wanao uwezo wa kuvitangaza zaidi vivutio vyetu kwa wananchi kutokana na utembeleaji wao.Vivutio ni pamoja na hifadhi za Taifa kama vile Mlima Kilimajaro,Tarangire,Saadani,Mkomazi na nyinginezo.

No comments: