|
Ziwa Magadi |
Ngorongoro:
Ni eneo pekee panapohifadhi wanyamapori na binadamu, mchanga
unaohama, palipogunduliwa nyayo za miguu na fuvu la binadamu wa kwanza.
Pia, kuna Ziwa Magadi ndani ya bonde refu na kubwa maarufu kwa jina
la ‘Ngorongoro Crater’ lililosababishwa na milipuko ya volcano zaidi ya
miaka 2000 iliyopita.
Mahali hapo si pengine popote, ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(Ngorongoro Conservation Area Authority – NCAA) iliyoanzishwa mwaka 1959
na kukabidhiwa majukumu makuu yafuatayo:
Kuhifadhi maliasili (wanyamapori, ndege na mazingira) zilizopo,
kuendeleza binadamu wenyeji (Wamaasai) na utalii katika hifadhi hiyo.
Ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,292, inapakana na
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) upande wa Kaskazini Magharibi na
miji ya Arusha, Moshi na Mlima Kilimanjaro upande wa Mashariki.