Pori
la akiba la Liparamba lipo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.Pori
hilo lililopo mpakani mwa nchi za Tanzania na Msumbiji,Lina ukubwa wa kilometa
za mraba 570. Hii ni asilimia 6.4 ya eneo la wilaya ya Mbinga ambayo ina jumla
ya kilometa za mraba 11,396. kiwango cha juu cha uoto wa asili wa misitu minene
ya miombo, yenye rangi ya kijani mwaka mzima.
Hifadhi hiyo inapakana na
Msumbiji kwa upande wa kusini, mto Ruvuma kwa upande wa mashariki, mito Lumeme
na Lunyele inapita ndani ya hifadhi hiyo na Kaskazini inapakana na milima ya
Goma la Mpepo ambayo ni miongoni mwa milima mirefu wilayani Mbinga.
Ndani
ya hifadhi ya Liparamba kuna aina mbalimbali za wanyama. Kuna palahala, swala
mkubwa(tandala) , boko, pofu, mbawala, mbuzi mawe, ngolombwe mnyama ambaye
anafanana na swala, chui, simba na fisimaji.Wanyama
wengine ni nyani-manjano, tumbili, nguruwe na ngiri. Vilevile kuna ndege
wa aina mbalimbali wakiwemo njiwapori,kanga na kware
Siku
za hivi karibuni wanyama kama tembo, pundamilia, nyati, nyumbu na mbwamwitu,
wameonekana katika pori hilo. Kuna baadhi ya wanyama wanahama kutoka Msumbiji na kuingia
Tanzania kwa kuzingatia hifadhi hiyo iko mpakani mwa nchi hizi mbili. Tanzania
inalenga kuboresha utalii kusini na kwamba hivi sasa watalii
wanachokifuata kaskazini pia wanaweza kukipata kusini kwa kuwa kuna utalii wa
aina mbalimbali.