Saturday 7 November 2015

PORI LA AKIBA LA LIPARAMBA KIVUTIO MAARUFU KUSINI MWA TANZANIA



  Pori la akiba la Liparamba lipo wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.Pori hilo lililopo mpakani mwa nchi za Tanzania na Msumbiji,Lina ukubwa wa kilometa za mraba 570. Hii ni asilimia 6.4 ya eneo la wilaya ya Mbinga ambayo ina jumla ya kilometa za mraba 11,396. kiwango cha juu cha uoto wa asili wa misitu minene ya miombo, yenye rangi ya kijani mwaka mzima.
     Hifadhi hiyo inapakana na Msumbiji kwa upande wa kusini, mto Ruvuma kwa upande wa mashariki, mito Lumeme na Lunyele inapita ndani ya hifadhi hiyo na Kaskazini inapakana na milima ya Goma la Mpepo ambayo ni miongoni mwa milima mirefu wilayani Mbinga.
   Ndani ya hifadhi ya Liparamba kuna aina mbalimbali za wanyama. Kuna palahala, swala mkubwa(tandala) , boko, pofu, mbawala, mbuzi mawe, ngolombwe mnyama ambaye anafanana na swala, chui, simba na fisimaji.Wanyama wengine ni  nyani-manjano, tumbili, nguruwe na ngiri. Vilevile kuna ndege wa aina mbalimbali wakiwemo njiwapori,kanga na kware
  Siku za hivi karibuni wanyama kama tembo, pundamilia, nyati, nyumbu na mbwamwitu, wameonekana katika pori hilo. Kuna baadhi ya wanyama wanahama kutoka Msumbiji na kuingia Tanzania kwa kuzingatia hifadhi hiyo iko mpakani mwa nchi hizi mbili. Tanzania inalenga kuboresha utalii kusini  na kwamba hivi sasa  watalii wanachokifuata kaskazini pia wanaweza kukipata kusini kwa kuwa kuna utalii wa aina mbalimbali.
       Kwa habari za Utalii na vivutio vya Tanzania TEMBELEA ZAIDI BLOG YETU

No comments: